Home » » Mwanamke adai figo yake aliyompa mumewe baada ya kuachwa

Mwanamke adai figo yake aliyompa mumewe baada ya kuachwa

 
Mwanamke mmoja aliyempa mumewe figo kuokoa maisha yake, anadai arudishiwe baada ya mumewe kumuacha hivi karibuni.

Andy Lamb alikuwa akisumbuliwa na tatatizo la figo na alikuwa anasaidiwa na huduma inayoitwa dialysis ambayo alikuwa akifanyiwa mara mbili kwa wiki ili kumpa uhai, mpaka pale mkewe Samantha alipomshawishi achukue figo yake moja.

Andy alifanyiwa operesheni ya kuwekewa figo mpya mwezi wa kumi mwaka 2009.

Baada ya miaka kadhaa baada ya kufanyiwa operesheni hiyoambayo ilikuwa ya mafanikiona kuokoa maisha yake, Andy aliamua kuachana na mkewe wa ndoa mwezi wa nane 2012.

Samantha amedai kuwa anajuta kumpa figo yake mtaliki wake huyo, anasema anamchukia sana na anatamani arudishiwe figo yake na ampe mtu mwengine.

Samantha mwenye  umri wa miaka 41 na mtoto mmoja amekuwa akiamini kuwa mumewe alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na shosti yake, lakini Andy alikanusha habari hizo ila amekili kuachana na Sammy

Wapenzi hao walikutana wakati wote wakiwa madereva kwenye kampuni ya magari binafsi ya wagonjwadriver, walianza mahusiano mwaka  2004, na kufunga kuoana mwaka 2007.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Tunashukuru kwa kuitembelea blog yetu, Acha maoni yako hapo chini, tafadhari usichafue hali ya hewa. Karibu tena!!

chatroom

Chatroom - socialize, be funny and make friends:)
 
Support : visit other blog here
Copyright © 2013. 247 Swahili News - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger