Home » » Dk.Slaa akerwa na vitendo vya Chadema Mbeya mjini, kisa hiki hapa

Dk.Slaa akerwa na vitendo vya Chadema Mbeya mjini, kisa hiki hapa

 
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk.Wilbroad Slaa, hivi karibuni kaatika viwanja vya CC Ilomba Jijini Mbeya, amesema licha ya mapokezi mazuri aliyooneshwa na wafuasi wake, lakini hajafurahishwa na jeneza lililokuwa limetengenezwa huku msalaba wake ukiwa na jina la mtu aliyehai Zitto Kabwe.

Amesema hali hiyo haipendezi kwasababu ishara ya jeneza inatisha hasa ikionesha taswira ya kumzika mtu aliye hai.

Alisema kumfukuza Zitto ni ishara ya chama chake kuthubutu kufanya yale watakayoyasimamia watakapoingia Ikulu ambapo yeyote atakayekiuka katika, atashughulikiwa na kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuchukua hatua kwa wanaokiuka sheria za nchi.

Kwa upande wake Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu), alisema amepata taarifa za Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuandaa kambi la vijana wa kuvuruga mikutano ya Chadema ambalo lipo katika shule ya Sekondari ya Chimala, inayomilikiwa na Umoja wa Wazazi wa CCM Mkoani Mbeya.

Taarifa hiyo imepuuzwa na baadhi ya viongozi wa CCM na UVCCM, ambao wamesema kambi la vijana hao ni kwa ajili ya halaiki ya sikukuu ya miaka 37 ya CCM Taifa, sherehe zinazotarajiwa kufanyika Jijini Mbeya na mgeni rasmi atakuwa ni Rais Jakaya Kikwete.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Tunashukuru kwa kuitembelea blog yetu, Acha maoni yako hapo chini, tafadhari usichafue hali ya hewa. Karibu tena!!

chatroom

Chatroom - socialize, be funny and make friends:)
 
Support : visit other blog here
Copyright © 2013. 247 Swahili News - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger