Home » » Lulu kupanda mahakamani Feb 17, 2014.

Lulu kupanda mahakamani Feb 17, 2014.

Mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambae anakabiliwa na kesi ya mauaji bila kukusudia ya mwigizaji Steven Kanumba anatarajiwa kuanza kujibu mashitaka yake kwa mara ya kwanza Februari 17, 2014 katika Mahakakama Kuu Tanzania Kanda ya Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya kesi za mauaji ya bila kukusudia iliyotolewa na Mahakama Kuu kwa kanda ya Dar es salaam, kesi hiyo ya Lulu itasikilizwa mbele ya Jaji Rose huku ratiba ikionyesha kwamba mshtakiwa akishasomewa mashtaka na kujibu, Mahakama itapanga tarehe ya kusikiliza maelezo ya awali dhidi ya kesi hiyo.

Januari 29 mwaka 2013 Lulu aliachiwa kwa dhamana baada ya kesi hiyo kubadilishwa hati ya mashitaka kutoka kwenye kesi ya mauaji kwenda mauaji ya bila kukusudia ambapo badiliko hilo lilimpa nafasi ya kupata dhamana.

Katika kesi ya msingi inadaiwa kuwa Aprili 7 mwaka 2012 Sinza Vatican jijini Dar es Salaam, Lulu alimuua Kanumba bila kukusudia.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Tunashukuru kwa kuitembelea blog yetu, Acha maoni yako hapo chini, tafadhari usichafue hali ya hewa. Karibu tena!!

chatroom

Chatroom - socialize, be funny and make friends:)
 
Support : visit other blog here
Copyright © 2013. 247 Swahili News - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger