Home » » Mnaigeria amuua mama yake huko Maryland

Mnaigeria amuua mama yake huko Maryland

Isaac Anya Ojiabo mwenye umri wa miaka 20 pichani juu, anashikiriwa na polisi kwa kosa la kumuua mama yake mzazi, Joy Ojiabo siku ya jumatano  Jan. 29th huko Forest Hill, Maryland.

Polisi wanasema walipokea simu ya 911 kutoka kwa mume wa marehemu, Anya Ojiabo, baada ya kumkuta mkewe hoi wakati amerudi nyumbani kutoka kazini.

Anya alipiga simu polisi na kuripoti kuwa Isaac ametoroka na gari la familia aina ya Lexus SUV baada ya kumjeruhi mama yake.

Polisi walifika eneo la tukio majira ya saa kumi na moja jioni na kumkuta Joy mwenye umri wa miaka 51, hoi kwa majeraha makali likiwemo moja la kuchomwa na kisu kifuani. Joy alifairki baada ya dakika 20 baadae.

Mtuhumiwa alikamatwa kesho yake Alhamisi kwenye makutano ya barabara ya Putnam na Crouse majira ya saa nne na nusu asubuhi .

Polisi pia wamesema walishapata simu mara tatu nyakati tofauti kuhusiana na marumbano kati ya mama na mtoto huyo.

Simu ya kwanza ni tarehe 7/3/2013 saa 2 usiku.

Ya pili ni tarehe 1/9/2013 saa 4 na dakika 12 asubuhi.

Na ya tatu ni tarehe 23/12/2013  saa 3 na dakika 45 asubuhi .

Hakuna arrest iliyofayika kutokana na matukio hayo matatu.

Isaac yuko rumande bila dhamana, na anatarajia kuhukumiwa kwa kosa la kuua na kujeruhi kwa kutumia silaha kali.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Tunashukuru kwa kuitembelea blog yetu, Acha maoni yako hapo chini, tafadhari usichafue hali ya hewa. Karibu tena!!

chatroom

Chatroom - socialize, be funny and make friends:)
 
Support : visit other blog here
Copyright © 2013. 247 Swahili News - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger