Home » » Serikali yafuta vyuo 10

Serikali yafuta vyuo 10

Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi yatankuvifuta vyuo 10 ambavyo havikusajiliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) .

Naibu Waziri wa wizara hiyo alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaama mbele ya Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na kuongeza kuwa kufutwa kwa vyuo hivyo ni kutokana na kutokufuata utaratibu wa kusajiliwa.

Alivitaja vyuo hivyo ni Media and Research Center, Vision Hotel and Tourism College, East Africa College of Hospitality and Tourism, The Africa Institute of Business Management , Aspiration Training Center, Dar es Salaam School of Hair Design, Media and Values Training Institute, Information Technology Training Center  vyote vya Dar es Salaam. Pia alikitaja Chuo cha Morogoro School of Medical Sciences cha Morogoro.

Katika hatua nyingine, waziri huyo alikiri kuwa kuna upungufu katika kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kupitia bodi ya mikopo.

Alisema kuna changamoto nyingi zinazoikabili bodi hiyo zikiwamo urejeshwaji wa mikopo kwa wanafunzi waliomaliza chuo, mfumo wa utoaji wa mikopo, ufinyu wa bajeti na makosa yanayotokana na wanafunzi kukosea kujaza fomu za mikopo
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Tunashukuru kwa kuitembelea blog yetu, Acha maoni yako hapo chini, tafadhari usichafue hali ya hewa. Karibu tena!!

chatroom

Chatroom - socialize, be funny and make friends:)
 
Support : visit other blog here
Copyright © 2013. 247 Swahili News - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger