Je wewe ni fashionista? Kunapenda shopping, kujaribu nguo mbai mbali, au kupangilia kabati lako kutokana na trend?♥ ...
Fashionista― inasemekana ni mwanamke anayeishi na kupumia fashion LOL. Unaposikia hilo neno kitu cha kwanza kufikiria ni stylish woman.
Okayyy, kutokana na taarifa nilizozipata kwa mtaalamu wa fashion, kuna aina tatu za fashionistas!.....Soma makundi hayo alafu ujiangalie upo wapi....LOL
Poser Fashionista.
Hayu ni yule mwanamke anayedhaniwa kuwa ni fashonista kwa sababu ya designer labels. Kila mtu anajua kama ana viatu vya Jimmy Choo, saa ya Gucci, bracelet ya Chanel [ambayo imeandikwa Chanel kwa msisitizo] na handbag ya Louis Vuitton. Ni yule bidada anayejionyesha kwa watu kuwa anavaa vitu vya designers tu na ana pesa [wapo wengi hapa mujini na ndio hao wanaishia kubeba sembe ili kumudu gharama...Just saying!]. Inasemekana mwanamke wa aina hii hupenda kujishow off lakini kiukweli ni fake! Ni mwanamke ambaye hana swaga zake binafsi 'personal style' na anafikiri kuvaa vitu vya majina makubwa duniani kutamfanya aonekane ni stylish na anaenda na wakati.[Red capert moments zinaharibu watu jamani lolest]
Huwa wanapenda sana chati na anajaribu kufanya hayo yote ili akubalike katika jamii ya wenye nazo 'luxury community' kitu ambacho a true fashionista would never do.
Budget Fashionista.
Huyu ni fashionista wa ukweli japokuwa hana pesa. Ni yule mwanamke anayependa kusoma magazeti ya fashion kama Vogue, Elle, InStyle and Harper's Bazaar na kuenjoy fashion anazoziona ndani ya magazeti hayo. Tatizo moja ni kwamba hawezi kumudu gharama za 'designer labels'. Anachofanya ni kuchukua current trends na classics na kujibunia style yake binafsi. Hutembela kwenye maduka ambayo anaweza kupata kinachofanana na kile alichokiona wenye gazeti au mtandaoni kwa bei poa au hata kushona. Anaweza vaa top ya sh 1000/= ikaoneka ya sh 20,000/=, ni wewe tu jinsi utakapyopangilia. Na kuna wakati ananunua kitu kimoja labda handbag au viatu vya designer na kuchanganya na vitu vingine kama nguo, hereni, blacelet vya bei chee, mchanganyiko wake huo unamfanya aonekane safi kabisa. Hii ni trick mojawapo ya ubunifu binafsi, unapata ile kitu roho inapenda na unapendeza gharama poa kabisa.
True Fashionista.
Huyu ni yule mwanamke mwenye pesa yake [sio za mawazo] na anaweza kumudu designer brands mfano Gucci,Chanel, CL, Dior, Oscar de la Renta, J.Mendel...you name it, lakini hajionyeshi kwa watu labda ugundue kama ni mtaalamu wa designer labels. Pia wakati mwengine wananunua vitu kwenye maduka ya kawaida kabisa as long ni good quality ― hawacomplicate mambo kama wakina bidada pale juu [posers]. Kundi hili ni wale wanawake anaweza kumatch kuanzia kisiginoni mpaka unyweleni bila kuchoka LOL. Anaelewa nini maana ya fashion na anapenda.
Kama wewe ni fashionista, kuwa na personal style yako. Usichechetuke na kitu sababu tu kina label fulani au umekiona red carpet―kama umekipenda nunua lakini sio sababu ya label. Kuna wakati unaweza kukutana na mtu kitu hakija mkaa fresh lakini madoido kibao kisa kina label ya Ralph Lauren... tuache ushamba na ulimbukeni...phew!!
Je wewe upo kwenye kundi gani hapo...wink!
0 comments:
Post a Comment
Tunashukuru kwa kuitembelea blog yetu, Acha maoni yako hapo chini, tafadhari usichafue hali ya hewa. Karibu tena!!