Home » » TBS wafanya operesheni ya kukamata nguo za ndani katika masoko ya Moshi

TBS wafanya operesheni ya kukamata nguo za ndani katika masoko ya Moshi

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, limeendesha operesheni maalumu katika masoko makubwa ya nguo za mitumba katika miji ya Moshi na Arusha yanayodaiwa kuwa wauzaji wakuu wa nguo za ndani zilizopigwa marufuku.

Operesheni hiyo iliyoanza katika masoko ya Klolotoni na soko la Kati na Unga Limited ya jijini Arusha, ilifanyika pia juzi katika masoko ya Meimoria na Mbuyuni  ambapo jumla ya Marobota matano yalikamatwa na kisha kuteketezwa katika dampo la Kaloloeni.

Angalia operesheni nzima ...bofya read more
Askari polisi wakikusanya nguo za ndani katika soko la Meiomoria wakati wa operesheni ya kukamata wauzaji wa nduo hizo zilizopigwa marufuku.
Mmoja wa wauzaji wa nguo za mitumba katika soko la Meimoria akiwa amejificha chini ya meza ya kuuzia nguo kukwepa askari polisi pamoja na maofisa wa shirika la viwango Tanzania (TBS).
Mwananmke huyo alitoka chini ya meza baada ya kubembelezwa na wenzake hata hivyo wakati askari polisi akimtaka kwenda kupanda gari la polisi mwanamke huyo alikimbilia tena chini ya meza hiyo,askari polisi wakalazimika kumuacha...hahaha!
Askari polisi akimsindikiza mwanamke mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja baada ya kukutwa akiuza nguo za ndani zilizopigwa marufuku katika soko la Meimoria mjini Moshi.
Mama huyo kiingia kwenye gari la polisi baada ya kukamatwa 
Askari polisi akimuhoji mmoja wa wauzaji wa nguo za ndani,juu ya uwepo wa nguo hizo katika stoo yake ya kuhifadhia Marobota ya nguo za mitumba.
Marobota yaliyokamatwa katika soko la Meimoria yakipakiwa katika gari tayari kwenda kuchomwa katika dampo la Kaloleni. Picha na Dixon Busagaga wa globu ya jami,Moshi.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Tunashukuru kwa kuitembelea blog yetu, Acha maoni yako hapo chini, tafadhari usichafue hali ya hewa. Karibu tena!!

chatroom

Chatroom - socialize, be funny and make friends:)
 
Support : visit other blog here
Copyright © 2013. 247 Swahili News - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger