Home » » Jamaa aliyedai kuwa yeye ni mtume Mohamad ahukumiwa kifo

Jamaa aliyedai kuwa yeye ni mtume Mohamad ahukumiwa kifo

Watetezi wa haki za binadamu wadai raia wa uingereza aliyehukumiwa kifo chini ya sheria ya Pakistan aachiwe huru.

Mohammad Asghar, raia wa Uingereza mzawa wa Pakistan, alifungwa mwaka 2010 baada ya kutuma barua ya wazi kwa viongozi mbali mbali akidai kuwa yeye ni mtume Muhamad.

Hakimu alitoa hukumu hiyo kali siku ya Alhamisi baada ya mshtakiwa kupandishwa kizimbani.

Mwanasheria wa Asghar amedai kuwa mteja wake ana matatizo ya akili hivyo hukumu hiyo sio sahihi.

Mbali na adhabu ya kifo, Mahakama pia imemuamuru Asghar kulipa fine ya rupee million moja za Pakistani ($10,000)

Taarifa  zinasema watu ambao wanakashifu au kumdhihaki mtume nchini humo, huwa wanavamia na kuuliwa na vikundi vya watu wenye hasira.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Tunashukuru kwa kuitembelea blog yetu, Acha maoni yako hapo chini, tafadhari usichafue hali ya hewa. Karibu tena!!

chatroom

Chatroom - socialize, be funny and make friends:)
 
Support : visit other blog here
Copyright © 2013. 247 Swahili News - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger