Home » » Baba ampiga mtoto wake na kumtoa uhai kwa madai hajafanana nae sura.

Baba ampiga mtoto wake na kumtoa uhai kwa madai hajafanana nae sura.

Mtoto Mwaru Lunard Sabil (9) aliyepigwa na kuumizwa vibaya na baba yake mzazi na kisha kulazwa katika Hospitali ya Wete, Pemba akipatiwa matibabu amefariki dunia.

Baba huyo mkazi wa Junguni Gando, Pemba, anadaiwa kumpiga na kumjeruhi vibaya mtoto huyo kwa madai kuwa hafanani naye sura., hivyo si mtoto wake.

Taarifa Zilizopatikana jana na kuthibitishwa na Daktari wa Wodi ya Watoto katika Hospitali ya Wete, Sada Juma Mbwana zilisema kuwa mtoto huyo amefariki dunia kutokana na maumivu makali aliyoyapata.

Baba mzazi wa mtoto huyo mwenye umri wa miaka 39 anashikiriwa na polisi kutokana na tukio hilo na anatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumatatu ijayo kujibu tuhuma zinazomkabili .
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Tunashukuru kwa kuitembelea blog yetu, Acha maoni yako hapo chini, tafadhari usichafue hali ya hewa. Karibu tena!!

chatroom

Chatroom - socialize, be funny and make friends:)
 
Support : visit other blog here
Copyright © 2013. 247 Swahili News - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger