Home » » Hii kali:Mwanamke amkana paka wake hadharani, asema ni shoga

Hii kali:Mwanamke amkana paka wake hadharani, asema ni shoga

Mwanamke mmoja nchini Nigeria aliamua kumkana paka wake wa miaka saba hadharani akidai kuwa ni shoga (gay)

Mwanamke huyo ambae jina lake halikuweza kutajwa, amesema paka wake amekuwa na tabia za kishoga kwani amekuwa akiwataka kimapenzi paka wenzake wa kiume.

Mwanamke huyo mwenye imani kali za kidini, amesema mwanaume na mwanamke wameumbwa kila mmoja kumridhisha mwenzie na si kinyume.

Ameongeza kuwa tabia ya paka huyo ni kinyume cha maadili na sheria za kibinadamu na wanyama.

Mwanamama huyo alitoa ofa ya anayemtaka paka huyo amchukue, lakini cha kushangaza hakuna aliyejitokeza.

Paka huyo mwenye jina la Bull, ameweka record ya kuwa paka wa kwanza shoga na kukanwa hadharani na mmiliki wake.

hahaha ukistaajabu ya Musa,utaona ya filauni
Share this article :

1 comments:

Tunashukuru kwa kuitembelea blog yetu, Acha maoni yako hapo chini, tafadhari usichafue hali ya hewa. Karibu tena!!

chatroom

Chatroom - socialize, be funny and make friends:)
 
Support : visit other blog here
Copyright © 2013. 247 Swahili News - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger