Home » » Hii laana: Mwanamke wa miaka 48 afanya mapenzi na watoto wa miaka 9-14 kwa zamu

Hii laana: Mwanamke wa miaka 48 afanya mapenzi na watoto wa miaka 9-14 kwa zamu

 
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Aretas Joseph, (48), mkazi wa kijiji cha Lesoroma tarafa ya Useri, wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, amehojiwa na polisi mkoani hapo kwa tuhuma za kufanya mapenzi na watoto wadogo wa kiume, wenye umri kati ya miaka 9 na miaka 14.

Inasemekana mwanamke huyo alikamatwa Januari 8, kufuatia ushirikiano ulioonyeshwa na majirani zake baada ya kupata taarifa ya tabia yake hiyo ambayo inaelezwa amekuwa akiifanya kwa muda mrefu.

Kulikuwa na tetesi mtaani kuwa mama huyo hufanya mapenzi na watoto wadogo, ndipo siku hiyo ya tukio majirani hao waliamua kuingia ndani kwake ili kujua ukweli wa tabia yake hiyo na kumkuta chumbani kwake akifanya mapenzi na watoto watatu.

Majirani hao walimvizia na kumfuma mama huyo, walitoa taarifa polisi na mama huyo kukamatwa na kufikishwa katika kituo cha polisi cha Rombo.

Watoto hao walipohojiwa walisema kuwa wapo Wanne na siku hiyo mwenzao hakuwepo na kwamba mama huyo amekuwa akiwachezea sehemu zao za siri huku akiwapaka mafuta katika sehemu zao hizo.

Watoto hao walidai kuwa mara baada ya kuwachezea sehemu zao za siri, huwa anawashawishi kufanya nao mapenzi kwa zamu huku wengine wakiendelea kumshikashika sehemu mbalimbali za mwili wake yakiwemo matiti yake.

Uchunguzi wa awali wa polisi unaonyesha ya kuwa mwanamke huyo amewahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na kijana mmoja aliekuwa amemaliza darasa la saba miaka mitano iliyopita na kujaliwa kuzaa nae mtoto mmoja.

Idara ya ustawi wa jamii imepewa taarifa ya mahusiano hayo na inafuatilia suala hilo.

Mhh! wanaume wote hao mjini jamani kufanya mapenzi na watoto...watu wengine kama wana mapepo
Share this article :

1 comments:

  1. Daaah huendaikawa mama huyo ni mgonjwa na ameathirika kisaikolojia

    ReplyDelete

Tunashukuru kwa kuitembelea blog yetu, Acha maoni yako hapo chini, tafadhari usichafue hali ya hewa. Karibu tena!!

chatroom

Chatroom - socialize, be funny and make friends:)
 
Support : visit other blog here
Copyright © 2013. 247 Swahili News - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger