
Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Ibrahim Jackson (24), amekutwa akiwa amekufa katika chumba cha mapumziko chuoni hapo bila mwili wake kuwa najeraha lolote.
Tukio hilo la kushngaza lilitokea saa 11:30 juzi jioni katika chumba namba 118 jengo namba D kilichopo mtaa wa Shaban Robert.
Marehemu alikuwa anasomea Shahada ya Usimamizi wa Kodi 'Tax Management' akiwamwaka wa pili.
Inasemekana marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kifafa kwa muda mrefu kabla hata hajajiunga na IFM.
Juzi jioni Ibrahim aliomba funguo kwa ajili ya kwenda kupumzika katika chumba kinachotumiwa kulala nawanafunzi kutoka nje ya nchi pindi wanapofika chuoni hapo kwa ajili yamasomo.
Baada ya tukio hilo, uongozi wa chuo ulitoa taarifa katika kituo cha polisi napolisi walifika katika chumba hicho na kumpeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa uchunguzi zaidi.
Pia wamewasiliana na wazazi wake waliopo wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya na taratibu za kuusafirisha mwili huo zitafanyika leo.
0 comments:
Post a Comment
Tunashukuru kwa kuitembelea blog yetu, Acha maoni yako hapo chini, tafadhari usichafue hali ya hewa. Karibu tena!!