Home » » Treni za juu kujengwa Dar hivi karibuni

Treni za juu kujengwa Dar hivi karibuni

Waziri wa uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe ameongea na TBC1 na namnukuu akisema ‘mradi unaanza wakati wowote mapema iwezekanavyo manake wenzetu tayari wanazo pesa hivyo ni sisi kukimbia tuanze mara moja huu mradi, barabara za juu za treni zinatengenezwa viwandani moja kwa moja hivyo kazi ni kuzisimika tu barabarani ndio maana haitochukua muda mrefu kukamilika’

Swali.....Je umeme wa bongo tunavyoufahamu na historia yake utafaa kuuwezesha usafiri huo wa Treni kufanya kazi yake? manake treni hizi za kasi zinatumia umeme. Lakini habari njema ni kwamba hawatotumia umeme wa TANESCO, watatumia umeme wa solar na vyanzo vingine vya umeme ili isitokee treni ikasimama katikati manake umeme ni lazima uwepo kwa saa 24′
Kazi hii ya ujenzi wa barabara za juu za treni na treni zenyewe Dar es salaam itafanywa na jopo la wawekezaji ambao tayari wameshakubali kuwa tayari kuifanya hii kazi kwa kuanzia Dar es salaam, baadae Arusha kisha Mwanza na kwa Dar es salaam.

Mradi huu kwa kuanzia utatoa ajira kwa zaidi ya watu elfu moja.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Tunashukuru kwa kuitembelea blog yetu, Acha maoni yako hapo chini, tafadhari usichafue hali ya hewa. Karibu tena!!

chatroom

Chatroom - socialize, be funny and make friends:)
 
Support : visit other blog here
Copyright © 2013. 247 Swahili News - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger