Home » » Wezi waiba milango, taa za gari na kuwapora wapita njia baada ya kutokea ajali eneo la tandale jijini dar

Wezi waiba milango, taa za gari na kuwapora wapita njia baada ya kutokea ajali eneo la tandale jijini dar

Vibaka wapora mali, milango, taa za gari na kuwapora wapita njia kufuatia ajali iliyotokea Tandale kwa Bonge jijini Dar es Salaam baada ya gari aina ya Nissan Patrol namba T479 BPJ kugongana na mwendesha Bodaboda ambayo haikujulikana namba zake jana usiku (Jumamosi).

Katika vurumai hiyo ambayo ilisababisha msongamano mkubwa wa magari, vijana wa eneo hilo walitumia fursa hiyo kung’oa milango na taa za gari hilo na vingine vilivyokuwemo ndani yake na baadaye waliendelea kuwapora wapita njia na watu waliokuwa kwenye daladala zilizokuwa zikipita hapo.

Dereva na mmiliki wa gari hilo, Alex Mutabazi (59) naye alichezea kichapo kikali kutoka kwa vijana hao. Polisi walifika eneo la tukio na kufanikiwa kuwatia mbaroni vijana kadhaa waliohusika na uporaji huo.
Dereva na mmiliki wa gari hilo, Alex Mutabazi (59) akiwa amejeruhiwa baada ya kipigo kutoka kwa vibaka.
 Kioo cha mbele nacho kimevunjwa
Hata vitu vilivyokuwa ndani ya gari hilo pia viliibiwa
Gari hilo likiwa limeondolewa mlango wa nyuma na vibaka
Vioo vya gari hilo vikiwa vimevunjwa.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Tunashukuru kwa kuitembelea blog yetu, Acha maoni yako hapo chini, tafadhari usichafue hali ya hewa. Karibu tena!!

chatroom

Chatroom - socialize, be funny and make friends:)
 
Support : visit other blog here
Copyright © 2013. 247 Swahili News - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger