Home » » Diamond kuwasomesha watoto walioshinda kucheza Ngololo East Africa international school.

Diamond kuwasomesha watoto walioshinda kucheza Ngololo East Africa international school.

Hatimaye Diamond ametimiza ile ahadi aliyoitoa siku ya tamasha lake na Christmas na leo amepost picha na kuandika ujumbe ufuatao:
Kama unakumbukumbu nzuri wakati nafanya tamasha langu la Christmass na Ngololo niliuliza mtoto atakae cheza vizuri Ngololo na kushinda nimpe zawadi gani?...na wengi walisema Nimuendeleze kielimu.... Hawa ndio washindi wetu walioshinda siku ile, ambao siku ya leo niliwapeleka Rasmi katika Shule ya East Africa International School iliyopo Mikocheni Dar es salaam ili waanze Masomo yao...Niliona ni vyema kama mtoto yupo shule ya kawaida nimuhamishe international school ili niweze kumsaidia elimu bora zaidi...Niushkuru pia uongozi Mzima na wanafunzi wa Shule ya East Africa International School kwa kuwapokea vizuri.

 

Simpo,mmoja wa waratibu akiwa ameongozana,na washindi wa ngololo Dancing
Diamond akisalimiana na mkuu wa shule Mercy Githirua
Alipata nafasi ya kuzungmza na wanafunzi na kuwausia mambo mbalimbali ya kimaisha....
Ofisin kwa mkuu wa shule tukimalizia taratibu za kuwaandikisha shule watoto
Wazazi wa watoto hao pia walikuwepo
Wakipitia form za usajili
Wazazi wakimshukuru Diamond
Wakisikiliza maelekezo kwa mkuu wa shule
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Tunashukuru kwa kuitembelea blog yetu, Acha maoni yako hapo chini, tafadhari usichafue hali ya hewa. Karibu tena!!

chatroom

Chatroom - socialize, be funny and make friends:)
 
Support : visit other blog here
Copyright © 2013. 247 Swahili News - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger