Home » » Mwimbaji Dencia akanusha kuwa cream zake sio za kujichubua

Mwimbaji Dencia akanusha kuwa cream zake sio za kujichubua


Mwimbaji Dencia alipata na maoni mbali mbali duniani ikiwa pamoja na tovuti maarufu kama MTO na BET kuwa cream zake "whitenicious"  ni za kujichubua na ni hatari sana.

Mwanadada huyo kutoka Cameroon alizindua cream zake hizo kama wiki mbili zilizopita na zimempatia umaarufu sana kwani kuna baadhi ya watu wanazipenda na kuna wanaozipinga wakidai kwanini mtu ajichubue na asibaki na ngozi yake asilia.

Dencia jana ametoa tamko kuwa cream zake sio za kujichubua bali ni za kuondoa makovu sugu yatokanayo na chunusi au mikwaruzo.

Dencia ambaye kabla alikuwa mweusi kama Kelly Rowland alianza kubadilika na kuwa kama Beyonce na sasa hivi kama unavyomuona kwenye picha hapo juu ni kama Kate Perry hehehe

Okayyyy people labda me sielewi maana ya Whitenicious.....nyie mnasemaje?

Tembelea tovuti yake HAPA
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Tunashukuru kwa kuitembelea blog yetu, Acha maoni yako hapo chini, tafadhari usichafue hali ya hewa. Karibu tena!!

chatroom

Chatroom - socialize, be funny and make friends:)
 
Support : visit other blog here
Copyright © 2013. 247 Swahili News - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger